RUMA AFRICA INVITE YOU TO WATCH EMMANUEL TV -TB JOSHUA LIVE

Thursday, August 16, 2012

RULEA SANGA AKIWA LOVE TANZANIA FESTIVAL AGOSTI 2012

Mwandishi: Rulea Sanga

Tamasha lililowakusanya watumishi wa Mungu kutoka Afrika na Bara la Ulaya. Kuna waimbaji kama Don Moen, Nicole Mullen na Reuben kutoka Marekani. Na Tanzania walikuwepo waimbaji wakongwe kama Christina Shusho, Upendo Kilahiro na Mch. Safari.

Mhubiri wa Tamasha hilo alikuwa Andrew Paula na kulikuwa na watumishi wengine wengi kutoka Tanzania

Katika mkutano huo kulikuwa na michezo mbalimbali kama Baiskeli na Pikipiki. Pia kulikuwa na shuhuda kutoka kwa mchekeshaji wa Tanzania, Masanja Mkandamizaji ambaye alitoa ushuhuda wake wa kuliwa miguu na funza akiwa kijijini kwake Njombe.

Uimbaji ulichukua nafasi kubwa sana, na ulikuwa baraka sana kwa Watanzania waliofika mahali pale.


Magari ya watu wa Mungu katika uwanja wa Jangwani


Blogger wenu (Rulea Sanga) nikielekea sehemu ya tukio


Andrew Paula akihubiri


Watu wa Mungu wakimsikiliza mhubiri


Blogger wenu nikipokea baraka kutoka kwa mhubiri Andrew Paula


Mwimbaji kutoka Marekani Nicole Mullen akiwapagawisha mashabiki wa Yesu


Man of God, Don Moen akimwimbia mwokozi wa maisha yetu Yesu Kristo


Nilipagawisha na uimbaji wa Nicole






Jamani salama huko??







No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...