RUMA AFRICA INVITE YOU TO WATCH EMMANUEL TV -TB JOSHUA LIVE

Monday, December 17, 2012

MGUSO WA KIPEKEE RULEA SANGA AUPOKEA KATIKA KANISA LA EFATHA MWENGE JUMAPILI YA 16.12.2012

Namskurum Mungu kama Mkurugenzi wa Rumafrica (Rulea Sanga) kwa kupata kibali cha kuhudhuria ibada ya Jumapili 16.12.2012 katika kanisa la Efatha la Nabii na Mtume Josephate Mwingira. Imekuwa baraka kwangu kutokana na mafundisho yaliyokuwa yanaendelea mahali pale. Nimepata kujua maana ya imani na faida zake. Ni hakika kama utasoma yale yote niliyokuletea naamini yataenda kufanyika baraka katika maisha yako. Na hivi ndivyo ilivyokuwa:
Rulea akitafakari Neno la Mungu lililohubiria siku ya Jumapili ofisini kwake baada ya kurudi tokea kanisani.



HAKIKISHA UNAYEMWAMINI YUKO HAI AU AMEKUFA?
Naomba tusome Warumi 10:17. Wiki iliyopita tulijifunza nini maana ya imani? Na inafanya kazi gani?
IMANI chanzo chake ni kusikia na kusikia huja kwa Neno la Kristo. Kuna watu wamesikia habari za mtume Fulani na kujenga imani yao kwake, na wengine wamesikia habari za makaburini na kujenga imani huko. Ili uonekane umeokoka, lazima uwe na imani, kwasababu huwakilisha kuwa huyu anaelewa nini na anajua nini?
Tusome tena Waebrania 11:1-6. Imani ni kuwa na uhakika wa mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasio onekana. Mungu anapoaanza kusikia Neno huwa ana imani na kuamini lile Neno.
Kuwa mwangalifu sana ma I,ani unayotembea nayo kwasbabu unaweza kuwa na uhakika na kitu kilichoharibika. Imani ni mtu amabye anahakika na jambo kuwa hili jambo linaenda kutendeka na unaenda kupata.

Imani haioni kitu ambacho hakionekani, bali huona kitu ambacho kinaonekana na hakipo. Mtu anayepaswa kuwa na uhakika wa mambo ni wewe na mimi tuliyeokoka. Imani inakuja kwa kusikia, Je, unasikia kushinda au kushindwa? Kama unasikia kushinda utashinda na kama unasikia kushindwa utashindwa. Kama ulisikia kwamba ndugu zako ni maskini na wewe utakuwa maskini, na akaamini, tambua hilo linaenda kufanyika kwasababu umesikia na umeamini.
Imani imejengwa kwa msingi wa Mungu. Mungu haonekani kwa macho lakini unasikia kuwa yuko Mungu na ndio maana up oleo kanisani na unamaamini hivyo hata kama hujawahi kumuona kwa macho yako.

Tunashinda mambo yetu kwasababu tunaimani kuwa Mungu atatushindia. Imani uliyonayo wewe ina nguvu na hakuna mafuriko au upepo utakaoondoa imani yako kwasababu imejengwa katika mwamba wa yesu Kristo..
Watu wengi wanafanya vituko vingi kama vile ufisadi wakiaamini ni nguvu zao. Kumbuka chochote unachofanya duniani ipo siku utatoa hesabu. Hakuna aliyeko duniani kwa bahati mbaya, jua Mungu anampango na wewe na anataka akutumie katika kazi yake.
Tunaokoka kwasababu tunampenda Mungu na sio kwa matendo mazuri tunayofanya, na pia imani yetu inatuhakikishia kuwa tuko na Mungu.
Imani haitaji kuwa na imani kubwa, ila ukisikia na ukakubali kwa kusikia kwako utashinda yale yanayokuzunguka. Imani tunayoongelea ni ya Mungu na sio imani zingine za kipagani na mashetani.
Imani inachukua vitu vilivyosirini na kuweka wazi. Imani hii ikiwa imemwamni Mungu, imani inaenda kwa Mungu na kujenga uhusiano, na uhusiano huo unakuja kwetu kwasababu tunamwamini.
Umimwamini Yesu atakupa uzima wa milele. Mtu mwenye imani hana hofu. Imani tuliyonayo inashuhudia kile tulichokiona, inaeleza tulichokiona. Imani yako haitaji kuwa na mtu mkubwa wa kufundisha ila inahitaji wewe kuichochea hiyo imani yako ndogo.

Imani ya mtu muda mwingine inasongwa sana. Unachotakiwa ni kupalilia imani yako na kusonga mbele. Linakuja jaribu pambana nalo na sahau na uendelee mbele na imani yako. Jaribu ulilonalo linakusukuma kwenye kusudio. Imani inaweza kukufanya hata adui zako kukufuata na kukutafuta uliko na kukupigia magoti. Unatakiwa kutopoteza imani uliyonayo kwasababu ina thamni sana.
Wewe mwenye imani, angalia sana unachosikia na unapaswa kujua sheria za Mungu. Unapokosa kuwa na imani wakati wa ugonjwa wako, kitu unachowaza ni kifo kwasababu huna uhakika kuwa Mungu anaweza kuponya.
Imani tuliyonayo ina nguvu na inashuhuda. Unapokuwa duniani na kuamni kuwa Yesu Kristo ni mwokozi wako, amini matatizo yako hayatakusonga tena. Yaliyoandikwa katika Biblia sio kwaajili ya historia ila ni kwa watu wa Mungu kuamini na watakachochukua katika Biblia wanenda kupona.
Unapovumilia mpaka mwish, ndipo unapookoka. Imani yako inatakiwa iwe na ujasiri. Unapoumwa vumilia na amini kuwa unaenda kupona. Imani alzima iwe na ujasiri ili uweze kushinda kwasbabu imani yetu ina mapmbano, kuna watu wanataka ushindwe..
Imani yako imejengwa kwenye Neno la Mungu ambalo ni sheria ya Mungu ambayo unatakiwa kufuata. Kila mtu aliyekuwepo hapa duniani awe ameokoka au hajaokoka lazima afuate sheria ya Mungu kutoka katika Biblia. Mungu anapoona ufuuati sheria ndipo unapoanza kupata mateso.
Huhitaji kuwa na imani kubwa sana bali kuwa na ujasiri wa imani yako kwasababu imani inakua na kuongezeka. Imani inakua na utukufu hadi utukufu. Kila unapoendelea kupanda ngazi, kuna jaribu utapitia.
Imani inakupa kufahamu yaliyokuzunguka na unakoendea. Imani inakusaidia kufahamu ulipo na unakoenda. Tunafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwasbabu tunaimani kutokana na maneno ya Mungu tuliyosikia na kuambiwa. Imani yako inakusaidia kufahamu kuwa wewe hakuna atakayekusumbua. Tambua ya kuwa aliyeokoka analindwa na yuko ndani ya Kristo.

Ukiwa na Kristo hakuna utakachopungukiwa. Lakini kuna jambo la kujiuliza, kwanini wewe unasema unaye kristo na shetani anakutawala? Ukiwa na imani unakuwa makini na mwendo wako. Imani sio kitu cha kuchezea, shetani anakuja kwako sio kwasbabu ni mzuri sana wa sura iala ni kutokana na imani yako. Mtu anapona kwasbabu ana imani. Yesu alipokuwa anawaombea wagonjwa alisema” Imani yako imekuponya, usitende dhambi tena” Dhambi zetu ndizo zinatutesa.
Imani haiku mbinguni ila iko kwako. Yeyote aliyeokoka yupo pale Yesu yupo, ambapo imani imekaa.
Mungu ukiwa naye hakuna atakayekuondoa chini. Ya jua hili kwasababu sisi sote tunalindwa kwa nguvu za Mungu. Unapokosea na kupatwa na matatizo ujue Mungu anakuchapa kwasababu umempoteza. Mungu anapokuchapa anakurudisha kwake kwasbabu anaona umepotea na unaenda kubaya zaidi.
Unapookoka unakuwa unasababisha matakataka kuoshwa upya. Unapokua kanisani usiwe unakuja kama desturi ila umekuja ili aondoe jambo linalokusumbua.
Imani inafanya vitu kuwa na ubora na haifanyi ovyo ovyo kwasababu yule aliye na asali ya Imani bora ni bora. Ili ufanye vitu vyenye ubora lazima uwe na imani ya kumpendeza Mungu. Imani ni kutafuta kwa kuleta vya sirini kuwa dhahiri.
Wale wamtafutao Bwana kwa imani atawapa utajiri ambao una furaha na kicheko. Munu aliyetuumba anataka watu wake kuishi maisha ya furaha na amani. Ukiwa na pesa mtafute Yesu kwa bidii. Wewe uliyeamuna kuwa na Yesu tegemea kuwa dhawabu.
Ulipookoka ulisema Mungu atakubariki, na umekaa mika miwili na umeona hakuna kubarikiwa na unatamani kuacha, nakuambia endelea kuchochea imani yako. Imani mara nyingi inaenda na maamuzi, nje ya maamuzi imani haiendi kufanya kazi.

Mungu amekuwa mwema kwako kutokana na imani yako yenye maamuzi na maamuzi ya kusaidia imani yako kutoyumba, kwa na ujasiri na kuwa na nguvu. Imani yako haitakiwi kuyumbishwa. Imani na maamuzi ni mwamba imara, haikupi kuona uharibifu ila kufajhamu kuleta kilicho bora siku zote
MUNGU AKUBARIKI
Mwandishi
Rulea Sanga
Mkurugenzi wa Rumafrica
+255 715 851523

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...