STEVEN KANUMBA AFARIKI DUNIA
_________________________________________________________
_____________________________________________________
_________________________________________________________
__________________________________________________
MAMA wa marehemu Steven Kanumba, ameanza kusumbuliwa na presha kiasi cha kulazimika kuwa chini ya uangalizi wa daktari.
_______________________________________________________
________________________________________________
_____________________________________________________
Muigizaji
wa filamu nchini Stephen Kanumba amefariki usiku wa kuamkia leo,baada
ya ugomvi na mpenzi wake huko nyumbani kwake Sinza Vatican.Mpenzi huyo
ametoroka na inadaiwa alimsukuma marehemu kwa nyuma na kudondokea
kisogo.Kanumba alilalamika maumivu makali ya kichwa ambapo alimwuita
mdogo wake ampeleke hospitali,lakini alifariki kabla hajafika huko.Mwili
wake umehifadhiwa Muhimbili.Source: Radio One
Mkurugenzi wa Global Publisher, Erick Shigongo akishirikiana na watengenezaji wa hema.
Ndani ya geti la marehemu Steven Kanumba
Blogger Rulea Sanga aliyevalia njano halkukosa msibani
H-BABA akihojiwa na waandishi wa habari
Wapenzi na ndugu wa marehemu Steven Kanumba nyumbani kwake
Mwigizaji Mainda wa pili kutoka kushoto akimfariji rafiki yake
Waigizaji wa filamu
Mwimbaji
huyu alielezea jinsi alivyoaagana na Marehemu Steve Kanuba
alipohudhuria katika bendi yake siku ya jana usiku, anasema marehemu
alimtania kuwa kesho ambayo ni leo kuwa atakuja na suti kali sana ambayo
ameinunua katika bendi yake
Mjasiliamali
Shigongo wa Global Publisher akihojiwa na waandishi wa habari, alisema
ni kitu chema kufanya kazi yako kwa kumkumbuka Mungu
Ruge wa Clouds FM alisema, ni pengo kubwa sana kwani katika sanaa alikuwa anahitajika sana
HISTORIA FUPI YA MAREHEMU STEVEN KANUMBA
HISTORIA YAKE:
Steven Charles Kanumbaa alizaliwa Januari 8, mwaka 1984 mkoani Shinyanga kabla ya umauti kumfiia Aprili 6, mwaka 2012.
Elimu
ya msingi alipata katika shule ya Bugoyi, na baadaye akajiunga na
sekondari ya Mwadui, kabla ya kuhamia Dar Christian Seminary.
Baada
ya kumaliza Kidato cha Nne Dar Christian, Kanumba alijiunga na
sekondari ya Jitegemee, Dar es Salaam pia kwa elimu ya Kidato cha Tano
na Sita.
Ni ni wakati huo akiwa Jitegemee Kanumba alianza shughuli za sanaa katika Kundi la Kaole Sanaa Group la Magomeni, Dar es Salaam.
Baada
ya kukomaa Kaole, Kanumba aliamua kuanzisha kampuni yake mwenyewe ya
filamu na hadi anakutwa na umauti alikuwa mwigizaji anayefahamika Afrika
nzima.
Ameshirikiana na wasanii wakubwa duniani kama Ramsey Nouah wa Nigeria na amefanya kazi na mastaa wengine kadhaa wa Nigeria.
Miongoni
mwa filamu ambazo alifanya ni Dar To Lagos, She is My Sister, Ancle JJ,
Oprah, Tufani, Johari, Gharika, Baragumu, Sikitiko Langu, Dangerous
Desire, Cross My Sin, Village Pastor, Family Tears na kadhalika.
Hivi karibuni, alikaririwa akisema atagombea Ubunge katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015.
Kanumba atakumbukwa na wengi sana kwa ucheshi wake- upole na ushirikiano mzuri na wenzake katika kazi.
Kifo
cha Kanumba ni pigo katika tasniya ya filamu Tanzania. Taifa
limempoteza mtu ambaye alikwishaanza kuitangaza vema nchi kupitia sanaa
hiyo na ambaye angetarajiwa kuitangaza zaidi katika anga za kimataifa
zaidi kupitia sanaa hii.
Nigeria sasa wanajua Tanzania sasa filamu. Nchi nyingi za Afrika zinajua sasa nah ii sehemu ya kazi nzuri kwa Kanumba.
Mwenyewe
aliwahi kukaririwa alifika hadi Hollywood hadi Marekani, ambayo ni
‘makka’ ya wacheza filamu. Kwa sasa mwili wa marehemu upo katika
hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam.
Mungu aiweke pema peponi roho ya marehemu. Amin.
___________________________
MH. RAIS JK KIKWETE ATUMA RAMBIRAMBI KWA FAMILIA YA MAREHEMU STEVEN KANUMBA
MH. RAIS JK KIKWETE ATUMA RAMBIRAMBI KWA FAMILIA YA MAREHEMU STEVEN KANUMBA
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com au press@ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania
–TAFF- kuomboleza kifo cha msanii maarufu nchini Steven Charles Kanumba,
aliyeaga dunia usiku wa kuamkia leo, Jumamosi, Aprili 7, 2012. Katika
salamu hizo, Rais Kikwete amemwomba kiongozi huyo wa TAFF kufikisha
salamu za rambirambi za dhati ya moyo wake kwa wana-familia ya Kanumba
na kwa wasaani wote nchini ambao wamepotelewa na mdau na Rais Kikwete
amesema kuwa ameshtushwa na kuzunishwa na kifo cha msanii huyo ambaye
amemwelezea kuwa msanii mahiri na mwenye kipaji kikubwa ambaye katika
uhai wa maisha yake mafupi na akiwa bado kijana sana amechangia kwa
kiwango kikubwa maendeleo ya sanaa ya filamu nchini na kupitia sanaa
hiyo kuitangaza Tanzania kimataifa. Amesema Rais: ”Nimepokea kwa mshtuko
na huzuni nyingi taarifa za kifo cha Ndugu Steven Charles Kanumba.
Kupitia filamu zake, ameburudisha na kuelimisha jamii yetu kwa namna
ambayo haiwezi kupimika. Alikuwa msanii mahiri na mwenye kipaji kikubwa
ambaye mchango wake mkubwa katika kuanzisha, kukuza na kuimarisha sanaa
ya filamu nchini hautasahaulika.” Ameongeza Rais Kikwete: “Ndugu Kanumba
pia ametoa mchango mkubwa katika kuitangaza nchi yetu ya Tanzania mbele
ya mataifa mengine kupitia sanaa ya filamu na uwezo mkubwa wa kisanii.
Tutaendelea kumkumbuka
kwa
mchango wake huo kwa nchi yetu.” “Nakutumia wewe Rais wa TAFF salamu
zangu za rambirambi na kupitia kwako kwa wasanii wote wa filamu na sanaa
nyingine kufuatia msiba huu
mkubwa
kwa fani yetu ya sanaa. Aidha, naomba unifikishie salamu za dhati ya
moyo wangu kwa wanafamilia wote. Wajulishe kuwa niko nao katika
msiba huu mkubwa. Waambie naelewa machungu yao katika kipindi hiki
kigumu cha msiba,” amesema Rais Kikwete na kuongeza: “Namwomba Mwenyezi
Mungu awape subira na nguvu za kuweza kuhimili kipindi hiki kigumu kwa
sababu yote mapenzi yake. Aidha, naungana na wana-familia na wasanii
wote nchini kuwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, aiweke pema peponi
roho ya Marehemu Steven Charles Kanumba. Amen.”
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Dar es Salaam.
07 Aprili, 2012
_________________________________________________________
ELIZABETH MICHAEL AU “LULU” ANAYESHIKILIWA NA POLISI KUHUSIANA NA KIFO CHA STEVEN KANUMBA
Sambamba
na jina lililotawala vinywani na akilini mwa watu wengi hivi leo, jina
lingine ni la Elizabeth Michael au maarufu kama Lulu ambaye kama
ilivyokuwa kwa Marehemu Steven Kanumba, naye pia ni muigizaji wa filamu
nchini Tanzania(Bongo Movies).
Lulu
anatajwa kuwa ndiye mtu ambaye mpaka dakika za mwisho alikuwa na
Marehemu.Inaaminika kwamba wawili hao walikuwa wapenzi ingawa
waliyafanya kwa siri kwani hivi karibuni wote wawili katika nyakati
tofauti kupitia kipindi cha Mkasi kinachorushwa kila Jumatatu na East
Africa Television, wote walikana kuwa na mahusiano na mtu
yeyote.Walisema wapo Single.
Hivi
sasa Lulu anashikiliwa na Polisi akiendelea kuhojiwa au kuwasaidia
Polisi katika uchunguzi wanaoendelea kuufanya kufuatia kifo cha
muigizaji huyo maarufu. Pamoja na kwamba vidole vingi kwa hivi sasa
vinamuelekea binti huyu mdogo lakini ambaye mara kwa mara amekuwa
akijaza kurasa za mbele za magazeti hususani yale “pendwa”, nadhani ni
busara zaidi kama tungeviachia vyombo vya dola(Polisi kwa wakati huu)
kufanya uchunguzi wao wa kina kwanza.
Tunaamini
kwamba Jeshi la Polisi litaweka hadharani taarifa kamili juu ya
uchunguzi wao. Tuendelee kumuombea Steven Kanumba apumzike kwa
Amani.Amina.
_____________________________________________________
MWILI WA MAREHEMU STEVEN KANUMBA KABLA YA KUINGIZWA MOCHWARI
Hii ndiyo sura ya ndugu yetu Steven Kanumba, mara baada ya kufikishwa hospitalini
MARAFIKI NA NDUGU WA MAREHEMU STEVEN KANUMBA NYUMBANI KWAKE SINZA VATICAN
Nyumbani kwa marehemu
MC Nova
Ndani ya geti-nyumbani kwa marehemu
Steve Nyerere aliyevalia Polo shirt ya mistari mweusi na mweusi
Mwigizaji a.k.a Chopa Mchopanga (katikati)
Msanii wa Bongo Flava, Noora wa tatu kutoka kushoto
Mvua akinyesha, alkini watu bado wako msibani
Gari la Marehemu Steven Kanumba
Mwigizaji wa Bongo Movie aliyekuwa muongozaji wa magari na kutoa tahadhari kwa wapenzi wa marehemu
Dogo akipigwa mvua kali
Mjasiliamali, Dotnata aliyenyoosha mkono wake wa kulia akipigwa mvua msibani
Mwigizaji a.k.a Judy akihojiwa Live Channel Five
Watu hawaamini kifo cha Kanumba (jembe)
Mwigizaji Johari akilia katika mahojiano na EATV
Mwigizaji maarufu sana, a.k.a Ray aliyevalia kofia akiwasiliana na jamaa baada ya mahojiano na waandishi wa habari
Nyumbani kwa Steven Kanumba
Blogger na Graphic Designer, Rulea Sanga (mwenye njano) akitafuta matukio kwaajili yako wewe mdau wa blogu hii
_________________________________________________________
PICHA ALIZOPOST MAREHEMU STEVEN KANUMBA TAREHE 6 APRIL 2012, NA KIFO CHAKE KIKAMCHUKUA SAA 7 USIKU WA TAREHE 7 APRILI 2012
**********
HAPPY 5TH ANNIVERSARY TMH,SAMBAMBA NA UZINDUZI WA DUKA/OFISI & TRAINING CENTER
SEHEMU YA DUKA LA NGUO TOKA KWA DESIGNER MBALIMBALI.
TULIOSAPOTI
MPAKA KITUO HIKI KUFIKIA HAPA KILIPO SOMA MAJINA HAPO JUU JINA LANGU
LIPO HAPO,KUSEMA UKWELI INAPOKUJA MAMBO YA KUSAIDIA JAMII NAJITAIDI
KUTOA NINACHOKUA NACHO MAANA HAPA HUKUMBUKA MANENO YA MWANDISHI ALBERT PINE..''"What we do for ourselves dies with us. What we do for others and the world remains and is immortal."
'' KANUMBA THE GREAT PIONEER MOTO WA VOLCANO'' NIKIWA KTK OFISI ZA TANZANIA MITINDO HOUSE.
Tembelea blogu yake: www.kanumbathegreat.blogspot.com
__________________________________________________
MAMA WA KANUMBA CHINI YA UANGALIZI WA DAKTARI
Kanumba
|
Dk.
Nassor Matuzya kutoka hospitali ya Mwananyamala, Dar es Salaam ambaye
amewahi kuwa Dakatri wa klabu ya Yanga, enzi za kocha Mserbia, Profesa
Dusan Savo Kondic ameiambia bongostaz joni hii kwamba yupo kwa ajili ya
kufuatilia hali ya Mama Kanumba.
“Mama anasumbuliwa na presha, inapanda sana, lakini namtibu na kwa sasa anaendelea vizuri,”alisema Dk. Matuzya.
Matuzya
alisema Mama Kanumba leo usiku atapelekwa hospitali ya Muhimbili, Dar
es Salaam kuuona mwili wa mwanawe kabla ya kuagwa na mazishi kesho.
Mama
huyo aliyewasili jana kutokea Bukoba, ameridhia mwanawe azikwe Dar es
Salaam, ingawa baba wa msanii huyo alipenda kijana wake azikwe karibu na
kaburi la babu yake, Mzee Kanumba huko Shinyanga.
Wakati
huo huo: Mwanamitindo Millenne Happiness Magesse ameongezwa kwenye
kamati ya Mazishi. Millene ameonekana tangu jana akiwajibika ipasavyo
kwenye msiba huo.
Kanumba
ataagwa kesho kuanzia saa nne asubuhi, viwanja vya Leaders, Kinondoni,
Dar es Salaam na kuzikwa kwenye makaburi ya Kinondoni.
Wakati
huo huo: Watu wameendelea kumiminika nyumbani kwa marehemu Sinza
Vatican kutoa rambirambi na miongoni mwao ni aliyewahi kuwa Mwenyekiti
wa Yanga, Wakili Imani Omar Madega.
Madega
alifika kutoa salamu zake za rambirambi na ubani kisha kuungana na
waombolezaji wengine. Mwanamuziki mkongwe, Kikumbi Mwanza Mpango ‘King
Kiki’ naye alifika. Chanzo;mama pipiro blog
_______________________________________________________
FIRST LADY MAMA SALMA KIKWETE AHUDHURIA MSIBA WA KANUMBA LEO
LEO
IKIWA NI SIKU YA TATU YA MSIBA WA KANUMBA, WAMESHAKUJA VIONGOZI KIBAO,
NA LEO JIONI TULIKUWA NA MKE WA PREZIDAR MAMAA SALMA, AMBAPO ALIKUJA TOA
MKONO WA POLE KWA WAFIWA
MSISITIZO::
KESHO
YATUPASA TUWAHI MAPEMA LEADERS CLUB KWANI SAA 4 SHARP SHUGHULI ZINAANZA
, KUTAKUWA NA PERFOMANCE ZA LIVE TOKA KWA WANAMUZIKI WALIOTOA SINGLE
MAALUM KWA MAREHEMU STEVEN KANUMBA, KUTAKUWA NA MISA NA KUMUAGA MAREHEMU
NA KISHA MAREHEMU ATAZIKWA MAKABURI YA KINONDONI KWENYE SAA KUMI N KWA
MUJIBU WA RATIBA
R.I.P KANUMBA
BAADA YA KUSAINI KITABU
|
ALIENDA MPA POLE MAMA MZAZI WA STEVE KANUMBA
|
WAOMBOLEZAJI NI WAKO WAKUTOSHA FAMILIA ,NDUGU NA MASHABIKI WA KANUMBA
________________________________________________
RAISI JAKAYA KIKWETE AWAFARIJI WAFIWA WA MAREHEMU STEVEN KANUMBA
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili nyumbani kwa marehemu Steven Charles
Kanumba Sinza 'Vatican' jijini Dar es salaam April 8, 2012 kwa ajili ya
kutoa mkono wa pole kwa wafiwa na kupeana mkonon na mdogo wake Kanumba.
|
Rais
Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo nyumbani kwa
marehemu Steven Charles Kanumba Sinza 'Vatican' jijini Dar es salaam
April 8, 2012 kwa ajili ya kutoa mkono wa pole kwa wafiwa.
|
Rais
Kikwete akiwafariji wafiwa nyumbani kwa marehemu Steven Charles
Kanumba Sinza 'Vatican' jijini Dar es salaam April 8, 2012 alikofika
kuomboleza nao kifo hicho.PICHA ZOTE NA FREDDY MARO WA IKULU
|
_____________________________________________________
___________________________________________________
........BABA WA KANUMBA ASHINDWA KUHUDHURIA MAZISHI YA MWANAE.......SHIBUDA AMWAKILISHA.......
MBUNGE
wa Maswa Magharibi, John Shibuda jana alimwakilisha baba wa msanii
maarufu wa filamu nchini marehemu Steven Kanumba katika mazishi ya
msanii huyo akidai kuwa baba huyo Charles Kusekwa Kanumba ameshindwa
kuhudhuria mazishi hayo kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya malaria na
shinikizo la damu na si matatizo yake na merehemu huyo. Kupitia
uwakilishi huo, Shibuda pia alisoma barua aliyoeleza kutoka kwa mzazi
huyo wa Steven Kanumba akieleza kushindwa kwake kufika kwenye mazishi
hayo na kwamba ametuma watoto wake na wakwe zake kumwakilisha. "Baba
yake Kanumba siku ya Jumamosi alikuwa anajisikia vibaya na alipokwenda
hospitali alipimwa na kukutwa ana malaria 15 na shinikizo la damu likiwa
180 - 140. Lakini pia ana matatizo ya miguu kwa muda mrefu, anatembea
kwa msaada wa baiskel,"alisema Shibuda. Akisoma barua hiyo Shibuda
alinukuu barua ya baba wa Kanumba akisema:"Salam, nashukuru wana kamati
ya mazishi ya mwanangu kwa kunitumia nauli ili niweze kuja kumzika mtoto
wangu. Lakini kutokana na maradhi yanayonikabili sitaweza kuja, ila
nawatuma wanangu Michael na Mjanael, pia mkwe wangu Chrisant Msipi
waniwakilishe. Matatizo yangu na mwanangu yalishakwisha." "Msianze
kuleta maneno yenu ya umbea umbea na uzushi eti hajafika kwenye msiba wa
mwanawe kwa kuwa hawaelewani huo ni uzushi, walishaelewana na alikuwa
na mawasiliano mazuri na mke wake mama Kanumba na ndiyo maana akatuma
wawakilishi wake,"alisema Shibuda.
____________________________________________________
HATIMAYE ELIZABETH MICHAEL AKA LULU APANDISHWA KIZIMBANI LEO KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA KANUMBA
Muigizaji wa Filamu nchini anaehusishwa na kifo cha Muigizaji Mwenzie,Marehemu Steven Kanumba,Bi Elizabeth Michael a.k.a Lulu amepandishwa kizimbani mapema leo asubuhi kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam kwa kusomewa mashtaka yake kuhusiana na kuhusika kwa kifo cha Muigizaji huyo nguli hapa nchini.
Elizabeth Michael amesomewa mashtaka hayo mbele ya hakimu Agustino Mmbando na wakili Elizabeth Kaganda ya mauaji ya Muigizaji wa Filamu nchini,Marehemu Steven Kanumba yaliyotokea huko sinza vatcan jijini Dar es Salaam april 7 mwaka huu.
Elizabeth Hakutakiwa kujibu chochote Mahakamani hapo kwani mahakama hii haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.
Kesi hiyo imeahirishwa na kupangwa kusikilizwa tena april 23 mwaka huu.
Muigizaji
huyo aliletwa mahakamani hapo kwa mwendo wa kasi kama mshale na kwa
ulinzi mkali na pia ndivyo alivyoondolewa Mahakamani hapo kiasi kwamba
hakuna hata mwandishi alieweza kupata picha ya Muigizaji huyo mwenye
tuhuma za mauaji Na kupandishwa katika gari ndogo nyeupe aina ya suzuki
grand vitara yenye nambari za usajiri T 848 BNV huku kwenye kioo nambari
zake zikisomeka PT 2565.Credits Michuzi Blog
________________________________________________________
NDUGU YETU PUMZIKA KWA AMANI STEVEN KANUMBA THE GREAT
Ni
majonzi makubwa sana kwa Watanzania wote sisi tulimpenda lakini Mungu
kampenda zaidi, inauma sana kwa kijana mdogo kama Kanumba kufariki
wakati alikuwa bado hajazitima ndoto zake .Mungu ailaze roho ya marehemu
Swaiba wangu Steven Kanumba ni mengi sana tuliyoyafanya mimi na wewe
katika gurudumu ili la sanaa bila kujali yote yaliyotokea ni kawaida ya
binadamu kutoelewana kama Baba na Mama wanafunga ndoa kanisani na
wanakula viapo vya utii mbele za Mungu lakini wanagombana na kufikia
hatua ya kuachana kwanini ishindikane kwetu ni hali ya kwaida katika
maisha binadamu kutofautiana mengi yanazungumzwa juu yangu ila kila kitu
mimi namuachia Mungu mimi ni mnyonge siwezi kupambana nanyi
mnaoniongelea vibaya maumivu nayoyapata juu yenu Mungu hatowaacha siwezi
kuzizuia hisia zenu kuzungumza yale mnayojisikia kuzungumza
Muda mfupi tu baada ya kufariki Steven Kanumba akiwa
kwenye gari lake la kifahari Lexus tangulia ndugu yangu sisi tuko nyuma
yako maana kila nafsi itaonja umauti. wadau nilikuwa kimya kwa
kutowaletea matukio kwa sababu ya shughuli zilkuwa nyingi sana katika
msiba nilikuwa kwenye kamati ya mazishi hivyo sikuwa nakipata muda wa
kutosha na sio watu wanavyofikiria jamani hata kama kuna matatizo ndio
katika maswala ya msiba hapana jamani mimi sijafikia hali hiyo yakuwa
na roho ya kinyama namna hiyo
Hapa tukiutelemsha mwili wa marehemu katika hospital ya Muhimbili ni mtu wa kwanza kufika katika eneo la tukio
Safari yetu ya mwisho binadamu wote mara ya kwanza nilipofika walikataa kumpokea pale hospital mpaka wapate PF 3 ndipo nilipowasha gari na kwenda Salenda polisi na kuwapata askari watatu ndipo tukapata fursa ya kwenda kumpuzisha marehemu
Tukimfunika macho maana yalikuwa wazi kama anasinzia
Hapa akiongea jambo na baadhi ya wanakamati ya mazishi
The Greatest nikimsikiliza Rais
_______________________________________________________
MCHAWI ADONODOKA NA UNGO JUZI KWENYE MSIBA WA MAREHEMU STEVEN KANUMBA NYUMBANI KWAKE SINZA..
_______________________________________
LUCRECIA KALUGILA (MAMA LULU) ASEMA ACHENI UMUHUKUMU MWANAE
Mama
mzazi wa msanii wa filamu anayehusishwa na kifo cha nyota wa filamu
nchini Tanzania, Steven Kanumba (28), Elizabeth Michael 'Lulu' amesema,
jamii isimuhukumu mwanawe kuwa amemuua ' Kanumba The Great'
Lucrecia
Kalugila amesema, wakati Kanumba na Lulu(18) wakiwa wanagombana
chumbani, walikuwa wawili tu, hivyo hakuna mwingine anayefahamu
kilichotokea hivyo watu wasimuhukumu mwanawe kuwa kamuua Kanumba.
Mama
huyo amesema, Kanumba ni mwanawe, na kwamba, hata yeye kifo cha msanii
huyo kimemsikitisha na kwamba, kama Kanumba angekuwa hai leo, angesema
namna walivyokuwa wanashirikiana.
Ametaka watu waache kuegemea upande mmoja kwenye tuhuma zinazomkabili Lulu, wasubiri sheria ichukue mkondo wake.
Amempa pole mama Kanumba, na kumshauri asiyafuate yanayosemwa mitaani kuhusu kifo cha Kanumba.
Mama Lulu amewaomba wanasheria wajitokeze kumtetea binti yake ili haki itendeke.
Lulu
yupo rumande tangu Jumamosi, akihusishwa na kifo cha Kanumba, na kwa
mujibu wa Polisi, atapandishwa kizimbani kujibu mashitaka ya mauaji.
KWA MUJIBU WA MDOGO WA MAREHEMU, SETI, LULU ALIKWENDA NYUMBANI KWA KANUMBA KUKAWA NA UGOMVI, WAKAINGIA CHUMBANI.
WAKATI WAKIWA HUKO, BAADA YA MUDA, LULU ALITOKA NA KUMUITA YEYE KUMUAMBIA KANUMBA KAANGUKA.
ALIPOENDA AKAMKUTA Kanumba KAANGUKA, AKAENDA kumuita DAKTARI WA KANUMBA ALIPORUDI HAKUMKUTA LULU.
Inadaiwa
kwamba, Lulu aligombana na Kanumba ambaye inasemekana alikuwa mpenzi
wake baada ya kukutwa akiongea na mwanaume mwingine, kwenye simu.
Hivi
karibuni Lulu alinukuliwa katika kipindi cha Mkasi kinachorushwa East
Africa TV 'EATV' akisema, hana MPENZI, na aliapia kiislamu kuthibitisha
kauli yake.
Kamanda
wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Charles Kenyella alinukuliwa akisema,
Kanumba alikuwa katika `ugomvi’ na LULU ambaye inasemekana kuwa alikuwa
mpenzi wake.
-----------------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------------
KANUMBA NA FREEMASONRY: MASWALI HAYA YANAWEZA KABISA KUTOA MAJIBU
PART II
KUHUSU KANUMBA KUNA MENGI YAMEZUKA KUWA ALIKUWA FREEMASON AU LA?
Mambo yafuatayo yanaweza kutusaidia kuamua bila maswali yoyote kuwa Steven Kanumba alikuwa Freemason ama la?
- Alama za Freemasons- Hapa ndio panaweza kutupa jibu kuwa Steven Kanumba au alikuwa kipenda kujiita Kanumba “THE GREAT”, alikuwa wa kipnda hicho ama la!
- Mazishi ya wanachama wa Kundi la Freemasons huwa yanakuwaje?- pia hapa panweza kutufumbua macho kujua uhalisia wa Kanumba na Freemasons kwa kuyachunguza mazishi yake yalivyokwenda.
- Sanduku/Jeneza lililioubeba mwili wa Mwigizaji nguli wa Tanzania katika Bongo Movies Steven Kanumba- linaweza kutupa ushahidi wa kutosha bila chenga.
Source: jaizmelaleo.blogspot.com/
_____________________________________________
VICENT
KIGOSI (RAY) THE GREATEST AMPA POLE MAMA WA MAREHEMU STEVEN KANUMBA
(THE GREAT) NA KUONYESHA JINSI ALIVYOJISHUGHULISHA KATIKA SUALA LA
KUMUWEKA MAHALI PA KUMPUMZIKA MILELE RAFIKI YAKE
Muda
ulifika wa Mama Kanumba kuwasili uwanja wa ndege wa Julius Kambarage
Nyerere maana wakati mauti yanamfika mwanae alikuwa safarini Bukoba.Mama
yangu mzazi(mwenye nguo nyeupe) ndiye aliyeongoza msafara wa kwenda kumpokea Mama Kanumba
Kamati ya mapokezi ikimsubiri Mama Kanumba kuwasili.
Muda ulifika na Mama akawasili na majonzi yakatawala.
Kilio na simanzi vilitawala uwanjani hapo(kulia) ndiye Mama yangu mzazi, Mama Mary Kigosi akimsaidia rafiki yake.
Pole sana Mama kwa msiba mkubwa uliokupata ninakuwaidi nitakuwa pamoja nawe kwenye shida na raha
Mama alishindwa kabisa kuzuia hisia zake mpaka kuzimia.
Njiani kuelekea msibani.
Tukimsubiri Mama mzazi wa Marehemu Kanumba.
Baada
ya kufika nikaenda kumpa pole,alilia sana aliponiona na kuniambia pacha
wako mwanangu yuko wapi umebaki peke yako? Niliumia sana.
Mazungumzo yakaendelea.
Akia kwa uchungu mkubwa sana. Pole mama.
Kesho yake nikaenda kutafuta jeneza la kumzikia ndugu yetu mpendwa.
Hili ndilo jeneza aliozikiwa Marehemu Steven Kanumba.
Baada ya kutoka kwenye majeneza nikaenda kuwachukua maskali kwa ajili ya postmortem
Tukiendelea kusubiria.
Nikiwa nimeshamaliza hatua zote.
No comments:
Post a Comment