RUMA AFRICA INVITE YOU TO WATCH EMMANUEL TV -TB JOSHUA LIVE

Tuesday, January 22, 2013

NABII NA MTUME JOSEPHATE AHUBIRI JUU YA UMUHIMU WA MAFUTA KUTOKA KWA BWANA YAKITIWA JUU YAKO. PIA MWAKA HUU NI MWAKA WA MASHANGILIO. RULEA ANATEGEMEA MAKUBWA KUTOKANA NA UTABIRI WA NABII NA MTUME J. MWINGIRA

Jumapili hii kulikuwa na maombezi kwa mama wajawazito, waliokoka, na watu wenye shida mbalimbali.SALAMU KUTOKA KWA MRS. NABII NA MTUME JOSEPHATE MWINGIRA.


Mungu wa Efatha anatushangaza, ukimtumikia utaona matunda yake. Tusome Zaburi 95:1-6, Njoo tumwimbie BWANA, tumfanyie shangwe mwamba wa wokovu wetu. Tuje mbele zake kwa shukrani, tumfanyie shangwe kwa zaburi, kwa kuwa BWANA ni Mungu na mkuu, na mfalme mkuu juu ya miungu yote. Mokononi mwake zimo bonde za dunia, hata vilele vya milima ni vyake. Bahari ni yake, ndiye aliyeifanya, na mikono yake iliumba nchi kavu. Njoo tuabudu, tusujudu, tupige magoti mbele za BWANA aliyetuumba.

Twende kwa Bwana na shukrani. Tatizo hata likiwa kubwa kwako litaenda kupungua kwani liko jina lenye nguvu (Yesu Kristo) wewe unatakiwa kuamini tu. Ubatakiwa kubadilika na kuwa na tabia mpya kwani ulipookoka uliachana na tabia mbaya na sasa uko katika himaya ya Yesu ya kuwa na tabia kama Zake.
Jinsi unavyotamka ndivyo unavyokuwa. Kwahiyo maneno yako yanaweza kuumba tabia Fulani maisha mwako. Kama wewe unatamka mema tu basi utakuwa mwema na kama unatamka na kufikiria mabaya utakuwa na matendo mabaya na mwisho wake ni mbaya.
Jizoeshe kuwa mtu wa shukrani kwa kile Mungu anakupa kwa siku na siku zote za maisha yako. Unapoenda mbele za Mungu toa sadaka yenye harufu nzuri mbele zake. Fungu lako ni agizo, kwahiyo huruhusiwi kula fungu la kumi.


TANGAZO LA MKESHA IJUMAA
Kabla hatujasoma Neno la Mungu, ningependa kuwajulisha yakuwa Ijumaa ni siku ya mkesha, kila mmoja akae mbele za Mungu  na andaa moyo wako kukesha na Bwana.

TAARIFA ZA UGENI ULIOFIKA EFATHA
Pia ningependa kuwajulisha kuwa leo kanisani kwetu tumetembelewa na wachungaji wengi sana kutoka Tanzania na nje ya Tanzania wamekuja kwaajili ya kushangilia na sisi katika kipindi hiki cha mashangilio. Siku ya leo ni siku ya mashangilio, na Yesu ametutangulia na kuwahi kanisani kabla yetu, kwa maana siku zote Yesu huwa anachelewa kidogo na sisi tunakuwa watu wa kumkaribisha.
SHUHUDA
Leo kuna mtoto wa kiume amezaliwa kanisani. Mama huyu alipata uchungu tokea Jumanne na akaenda hospitalini na kuambia atafanyiwa operationa (atajifungua kwa kisu). Mama huyu alikataa ushauri wa daktari na kuamua kuja kanisani Efatha. Alipofika hapa yalifanyika maombi. Baada ya maombi kuisha mama alijifungua mtoto wa kilo tatu na nusu kanisani kwa njia salama. Alipoingilia mtoto ndipo alipotokea. Tuunamshukuru Mungu.
Ninachotaka kuwaambia kuna siku watu watazaa humu kanisani na mtashangaa vitoto vikilialia.
Siku moja Yesu alipotoka safari kuelekea Yerusalemu, alisema “Mtamuona mwana punda mfungueni na mkiulizwa, semeni, Bwana anamhitaji” Hata wewe ukiona mtu amefungwa basi unatakiwa kumfungua na ukiulizwa, sema Bwana anamhitaji. Mkiona mtu anauhitaji, mpeni na msiwe wanyimi. Nimemuomba Bwana atoe kile kilicho chake na awape ninyi wenye uhitaji..Pokea kwa jina la Yesu!!!. Na kile nilichonacho Nabii wenu Mungu akupe na wewe kwa jina la Yesu.
Nimemuomba Mungu anipe wenye Roho ya Efatha, wale wenye uhitaji wa kumtafuta Mungu kwa akili zao na mali zao.

MAONO
Nabii na Mtumwa Josephate Mwingira alimuona mtu mwenye mateso katika ulimwengu wa Kiroho na alipomuita kwa jina yule mama alijitokeza huku akilia machozi, kwani hakutegemea kabisa kuitwa. Na hivi ndivyo alivyosema

Kuna mama mmoja anaitwa Maria John, nasikia sauti hii kutoka mbinguni ikiita. Sasa unaondolewa na mizigo yako. Nakuomba uje mbele haraka sana. Na wewe unayekandamizwa uondolewe na mikandamizo yako.
Kuna wakati Mungu anashughulika na watu bila ya wewe kujua. Unaweza kuona mtu anafanikiwa na hujui ni kitu gani kinamfanya huyu mtu afanikiwe, ila Mungu peke yalke ndiye anayejua.
Kanisani ni mahali pa kukaa na watakatifu bna sio na wenye mapepo. Mapepo hukaa kwa wanyama hasa nguruwe, kwahiyo mapepo kama mpo kanisani nawaamuru kuondoka na mkaishi katika sehemu zenu chafu.
SOMO LA JUMAPILI KUTOKA KWA NABII NA MTUME JOSEPHATE MWINGIRA.
“ROHO WA BWANA YU JUU YANGU”

Tusome Luka 4:18, Roho wa Bwana yu juu yangu, kwa maana amenitia mafuta kuwahubiria maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, vipofu kupata kuona tena, kuwaacha huru waliosetwa, na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubariwa.
Roho wa Bwana yu juu yangu kwasababu amenitia mafuta ya furaha. Wakati wengine wanabarikiwa, mimi lazima nibarikiwa zaidi yao kidogo. Mungu anasema hamtakuwa mkia bali vichwa, na wewe utakuwa unapokea na kuwapa watu wengine.
Mwisho nasema, naomba ukae mbali na dhambi kwani utaona mashangilio. Mwamini Mungu kwani mwaka huu ni mwaka wa mashangilio.
MUNGU AWABARIKI
Mwandishi
Rulea Sanga

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...