RUMA AFRICA INVITE YOU TO WATCH EMMANUEL TV -TB JOSHUA LIVE

Sunday, January 13, 2013

RULEA SANGA AZIDI KUNENEPA NA CHAKULA ANACHOPATA KATIKA NYUMBA YA BWANA YA NABII NA MTUME JOSEPHATE MWINGIRA KATIKA KANISA LA EFATHA. JUMAPILI HII NILILISHWA JUU YA "ROHO WA BWANA YU JUU YANGU" KATIKA KIPENGELE CHA "MACHO KUONA TENA"



ROHO WA BWANA YU JUU YANGU
Ukiwa umeokoka uwe mmoja wa watendaji na usiwe mtu wa kuchungulia na kushangaa wenzako wanaofanya kazi ya Mungu, jihusishe kwa kufanya kazi ya Mungu kwa vitendo na usiwe mtu wa kupokea tu. Kama wewe ni mwimbaji basi imba sana, kama wewe unahusika na mitandao basi sambaza Neno la Mungu, kama wewe ni mchungaji fanya kazi ya Bwana kama hutakuja kufanya tena n.k.
Roho wa Bwana yu juu yangu kwasababu Bwana amenipaka mafuta ya furaha. Mwaka huu ni mwaka wa mashangilio na kila siku ni shangwe.
MACHO KUONA TENA.
Ili macho kuona tena kuna mambo ya kuzingatia ambapo Neno linaeleza kuna mambo unayahitaji:
MOJA: (Yohana 1:3). Neno linakusaidia kuona. Unatakiwa kutenga muda wako kwa siku na kutafuta sehemu tlivu na anza kusoma Neno la Mungu na kuomba kwa muda wa siku kama nne.
Ukiomba jambo lolote lolote kwa Baba na Yeye atalifanya, ili BABA atukuzwe
(Yohana 14:13). Kila aminiye Mimi nia kazi ninazozifanya na yeye atafanya zaidi. Yangu, na kila anachokiomba kwa jina langu, Mungu atafanya na jina la Bwana litatukuzwa.
Pata nafasi ya kutulia na kupata Neno, na katika Neno kuna chakula cha uzima. (Yohana 6:32), hata kama umechoka kimwili, nenda kusoma Neno la Mungu na ukifanya hivyo mwili wako unahuwishwa na unatiwa nguvu ya kusoma Neno la Mungu na kusonga mbele.
(Timotheo 2:3), Neno ni pumzi ya Mungu na hutuongoza, hutuadisha ili watu wa Mungu wawe kamili. Kwahiyo tunaweza kusema Neno la Mungu linafanya yafuatayo
(a)    Linakuongoza
(b)   Linakuadibisha
(c)    Linakukamilisha
Ili mtu awe kamili, amekamilishwa kutenda mema. Unatakiwa kuwa mwema mpaka jirani yako aone kweli umeokoka. Na sio matendo yako machoni pa watu ni vituko na wanabaki wanashangaa kuwa huyu kweli amekoka!!
Katika shida unayopitia, kibu lake liko kwenye andiko, haupaswi kupata shida juu ya shida yako unayopitia. Wewe soma neno la Mungu na mwisho wa siku utapata jibu la shida yako.
Waume mnapaswa kuwapenda sana wake zenu kama Yesu alivyoupenda ulimwengu na akafa ili mimi na wewe tupone. Miwanyanyase wake zenu kwani hao ndio waliokufanya mpaka sasa unaonekana hivyo. Kama mama yako angekuwa hakupendi,hangeweza kukuzaa, lakini aliamua kukaa na wewe mpaka ukazaliwa.
Kabla maumivu au jambo lolote halijafika angalia Neno. Unaweza kutambua jema kama una Neno la Mungu. Neno la Mungu linakupa mwisho wa jambo kuwa mwema na kukupa ushangilio.
Magonjwa na maumivu mengi yanaletwa kama huna Neno. Unapokuwa na Neno la Mungu linakukinga na wale wabaya wanaoweza kusababisha magonjwa kwako. Kila watakapotaka kukuingilia wanakutana na ulinzi wa Neno.
(Timotji 2:4:6-7), Hufi ghafla, bali unaaga na kutangaza kifo mapema. Kifo cha mwamini si cha ghafla ila unapata muda wa kuagana na wenzako. Yesu aliumaliza mwendo na  hakuishi njiani. Kuna watu wengine hapa kanisani Efatha tunawapa Uaskofu na wakipata baada ya muda wanaacha nap engine kuhama kanisani. Ukipewa kazi ya Mungu fanya kwa uaminifu mpaka mwisho wa mwendo ili ukabidhi kwa ushindi.
Unapoenda kusoma Biblia unaendelea kulinda imani yako. Mtu mwenye Imani hawezi kuliwa na shetani na shetani hawezi kumsumbua. Kama una nguvu ya Mungu huhitaji kulia ila mshukuru Mungu na kumuombea mmbaya wako anayekujia.
Maumivu na mateso mnayoyapata ni kwasababu hamfuati maelekezo ya Mungu mnayoambiwa na watumishi wenu na yaliyomo katika kitabu Kitakatifu yaani Biblia.
Neno la Mungu linakupa ujasiri wa kuomba. Kitu cha muhimu sio ushuhuda ila mtu kupata kuokoka. Yesu hakuja kwaajili ya wagonjwa ila alikuja kuwaokoa. Makuhani waliponya ila hawakuwaokoa watu mpaka Yesu alipokuja. Unatakiwa kujiuliza, umesababisha wangapi kuokoka..?
(Yohana 1;5:14-15), ndani ya Neno unapata ujasiri wa kitu unachosema. Neno linasema ukiomba lolote kwa jina la Langu, mimi Bwana nitatenda. Neno la Mungu linakupa yale akukarimiaye.
(Wakoritho 1:2:12), ukiangalia Neno ndipo unajua nini Mungu amekukeremea. Mungu hajibu maombi yasio na Neno lake. Omba kulingana na neno la Mungu. Mungu haangali umaskini wa mtu bali anaangalia moyo wake unaohitaji utajiri. Mungu anaangalia mambo yafuatayo huko ndani ya moyo wako ili akupe utajiri:
(a)    Kusudi la Mungu. Ukipata utajiri utakuwa na kusudi gani mbele za Mungu?
(b)   Utafanya kazi ya Mungu. Kama utapewa huo utajiri, utafanya kazi ya Mungu au ni kwaajili ya mahitaji yako nay a familia yako?
(c)    Unaupendo wa Mungu. Ukipata huo utajiri utazidi kuwa na upendo wa Mungu, au ndo kwanza utawachukia wenzako pamoja na kupuuzia kazi ya Mungu?
(d)   Matumizi yako ya kila siku. Je, matumizi yako yataendana nay ale ya Mungu?
Mungu anaangalia Neno linasemaje huko ndani yako. Unaongea ubinafsi wako au ukuu wa Mungu?

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...