Siku ambayo nilibahatika kukaa na bloggers wenzangu kama Sam Sasali, Victor wa Hosannainc na Uncle Jimmy. Kikao chetu kilihusiana na jinsi ya kumpromoti mwanamuziki wa injili Tanzania, Christina Shusho. Mwimbaji huyu alikuwa amechaguliwa katika mashindano ya kumtafuta mwimbaji bora wa nyimbo za injili. Mashindano haya yalifanyika Marekani.
Kama bloggers tulikaa kwa pamoja ili kumtangaza Christina Shusho kwa kupitia mitandao tunayomiliki. Kikao chetu kilifanyika Mwenge karibu na Mlimani City Dar es Salaam siku ya 12 June 2012. Kipindi hicho blogger wenu nilikuwa na mwezi mmoja toka nimetokea kwa Nabii TB Joshua Nigeria.
Blogger na Mkurugenzi wa Ruma Africa, Ruleangu wana weka mambo sawa
Sam Sasali aliyesimama akihakikisha mambo yanasonga
Victor na Jimmy wakisikiliza kwa makini, maneno kutoka kwwa Sam.
No comments:
Post a Comment