RUMA AFRICA INVITE YOU TO WATCH EMMANUEL TV -TB JOSHUA LIVE

Tuesday, January 1, 2013

EFATHA YAZIDI KUMULISHA CHAKULA BORA MKURUGENZI WA RUMAFRICA RULEA SANGA. JUMAPILI HII KULIKUWA NA SOMO LA ROHO WA BWANA YU JUU YANGU.

Ibada ya jumapili iliongozwa na Nabii na Mtume Josephate Mwingira, mmbeba maono ya Efatha Tanzania na dunia kote. Watu tulibarikiwa sana na somo lake lenye kubadilisha maisha yetu. Kulikuwa na ujulisho wa shule mpya ya Eaftha. Nabii na Mtume alituhimiza watu kufika katika mkesha wa 31.12.2012 (jumatatu) bila ya kukosa. Waumini tulihimizwa kuvaa Tshirts ziliandikwa KUSANYIKO LA 2012 ambazo zinauzwa hapo kanisani.

Nisiwachoshe tuangalia na tusome yale yaliyotamkwa madhabahuni:


Nabii na Mtume Josephate Mwingira wa kanisa la Efatha-Mwenge

UTANGULIZI NA MATANGAZO
Kanisa la Efatha linakuomba wewe mwenye mtoto unayetaka mtoto wako kujiunga na Pre and Primary School. Tarehe 3.1.2013 kuanzia saa 3:00am – 9:00pm fika kumuandikisha mwanao. Pre- Primary ni kuanzia umri wa miaka 3 na Primary ni miaka 7 na kuendelea.
Vitu vya kujanavyo ni
  1. Cheti cha kuzaliwa au kadi ya Clinic au cheti cha ubatizo
  2. Picha za Passport size
  3. Tshs. 10,000 kwaajili ya kununulia fomu
Kama kuna mwalimu anaweza kufundisha, Efatha inamhitaji.
Mwaka 2013 tumedhamiria kuwa na shule ya watoto. Elimu tunayotaka kuifanya ni nyingine, tunawaandaa watoto kufika mbinguni. Tutafundisha masomo mengi kama
  1. Jiografia – Watajifunza elimu ya uumbaji
  2. Historia – Watajifunza Ukombozi kwa kujua ametoka mahali pa chini na anaelekea mahali pa juu
  3. Sayansi – Elimu kuhusu Mungu, kwa mfano Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na nchi.
 
Mtoto baada ya kumaliza atajiona yeye ni mtu wa tofauti sana. Tutaanza na shule ya Principle, tutakuja Primary na baadae kumalizia na Secondary. Mungu akituwezesha tutakuwa na University.
Tunandaa kitu cha kujenga na sio cha kubomoa.

Nikupe ushuhuda wangu kama Nabii Mwingira, Mimi nilipoanza huduma sikuanza na kuomba misaada kutoka kwa wazungu au mtu yeyote yule, ila ni bidii zangu. Nilianza huduma bila kuangalia huduma za watu wengine au katiba za watu wengine.
Nilikuwa wa kwanza kufungua Chuo Cha Biblia Tanzania. Nilikuwa muhubiri wa kwanza kuweka order. Katika kanisa langu Askofu sio boss, nah ii tofauti na makanisa mengine ambapo Askofu ni boss. Katika Efatha kazi kubwa ya Askofu ni kuswaga mapepo. Mitume wana kazi ya kuongea na Mungu na kuleta habari kanisani na kanisa likipata habari linapeleka mitaani
Tunatakiwa kuwafundisha watoto katika level ya Kimbinguni. Paulo alipata kufahamu alipokuwa chini ya mwalimu. Watoto wetu tutawafundisha huku tukifananisha na maneno yaliyoko katika Biblia, kwa mfano:

A=Alfa
B=Efatha
I=Imani
O=Omega
U=Ufalme
Kinachowaponza Watanzania kuwa mafisadi ni ujinga, hawamjui Mungu. Watanzania walifundishwa kudanganywa kuanzia uongozi wa awali mpaka uongozi tulionao. Tuliambiwa kuwa kila mtu ni sawa wakati viongozi hawa wakiwa wanatembelea magari, wanatumia TV, wanalipiwa nyumba za kuishi wakati wengine hawana hivyo vitu. Viongozi awali walitukataza kumiliki TV, magari vitu vya thamani wakati wao wanamiliki.
Katika dunia kuna uzao wa:
  1. Kiungwana
  2. Kishenzi
  3. Kifalme
Ukitoka katika uzao wa kishenzi na wewe unakuwa mshenzi. Ukitoka katika uzao wa Kifalme na wewe unakuwa mfalme. Kwa mfano Musa aliambiwa atafute mtu wa kumsaidia kati ya watu wenye hekima.
Tunatakiwa kuiombea Tanzania kupata watu wa kuiongoza nchi hii. Kama kuna watu washenzi ni wale wanaowadharau walimu wao waliowafundisha na mpaka sasa wanaitwa wasomi, huu ni ushenzi.
Ukisoma Biblia inakupa mwanga wa kujua watu gani wanatakiwa kuwa na madarakani.
Uzao wa kiungwana, hata ukikosea una tabia ya kujikosoa na kukiri kuwa hapa ameshindwa, lakini uzao wa kishenzi ukikosea unapigana.
Uki associate uzao wa kishenzi na uzao wa kiungwana automatically unakuwa na uzao wa KIUNGWANA. Hata wewe ulipokuja kanisani na kuungana na Nabii wako Mwingira, Mungu amekukabidhi kuwa Askofu na sasa unaswaga mapepo wakati zamani ulikuwa hufanyi hivyo..
Mwakani uwe na mawazo ya kujua kuwa kuna mahali umetoka na mahali unaenda. Bwana anasema unaweza mambo yote katika yeye akupae nguvu.
Leo hata kama walisema mengi mabaya kwako kama vile kutoa au kuolewa, wameshindwa na utatoboza. Ndivyo Mungu atakavyofanya, kama wewe utakuwa mchovu utapata mchovu mwenzako wa kuishi naye.
NENO KUU LA JUMAPILI
ROHO WA BWANA YU JUU YANGU.
Roho wa Bwana yuko juu yako kwa kupakwa mafuta na Bwana, kwasababu nimependa haki na kuichukia dhuluma (Zab: 45:7). Kwa kuchukia dhuluma, Bwana amepaka mafuta lakini yamezidi kidogo kuliko ya mwenzako.
Shetani mara nyingi hafurahi sana anapoona una raha na kufurahi, bali hufurahi sana anapoona unalia na yeye huongezea.
Kuna dada mmoja alikuwa na kilio na maumivu kila siku. Nikaamua kumfanyia maombezi na akadondoka. Karibu nusu saa anajamba tu, na baada ya nusu saa mbele akawa mzima. Mwaka uleule akapata mtoto. Alisumbuliwa kwa muda wa miaka kumi bila ya kupata mtoto.
Angalia mafuta ya furaha utayapataje?
  1. Tusome Zab:91,  kwa kuteguliwa mitego ya shetani na Mungu. Kila wanapotega wewe unavuka. Usilie unapoona kuharibikiwa kwako. Unapoona mlango umefungwa, Bwana anafanya mlango wa pili. Acha kulia kwa kitu kilichopita, huo sio msiba wako. Ukiona msiba wako umekuja peleka msalabani, hata kama watasema hutafika, wewe waambie nitafika. Wakati watu wanasema usiende kanisani Efatha, wewe wambie lazima nifike. Mwanamke aliyetokwa damu hakujali na kuanza safari ya kwenda kwa Yesu ili agues pindo la vazi lake Yesu. Bathelomeo alisikia Yesu anapita akaanza kusema “Yesu mwana wa Adamu unirehemu’” watu wakamzuia huku wakimchangia pesa, lakini yeye akazidi kumwita Yesu huku akichukua pesa zao. Yesu akamuuliza unataka nikufanyie nini? Akasema nataka kuona, Yesu akampa uponyaji na kuweza kuona.
Mungu ametupa mafuta sio ya msiba bali ni ya furaha. Unavyotembea hapa duniani, tembea na kujiona wewe umepakwa mafuta zaidi yaw engine. Anza kuwaza katoika akili yako kuwa umepakwa  mafuta.
Furaha ya Nabii na mtume Josephate Mwingira ni kuona wewe unafuraha kwa maana furaha yako ni maendeleo yako  na shetani anachukia.

MUNGU AKUBARIKI

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...