RUMA AFRICA INVITE YOU TO WATCH EMMANUEL TV -TB JOSHUA LIVE

Thursday, November 28, 2013

RUMAFRICA YATENGENEZA TANGAZO LASHEREHE YA MIAKA SABA YA UREJESHO KANISA LA RGC TABATA CHANG'OMBE KWA MTUME PETER NYAGA NA MGENI RASMI NI WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA TANZANIA MH. MIZENGO PINDA


· Ni katika sherehe ya kihistoria kutimiza miaka saba ya Urejesho

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mizengo Pinda, Jumamosi ya wiki hii, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe maalum ya kutimiza miaka saba tangu kuanzishwa kwa kanisa la RGC Tabata Chang’ombe jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika mahojiano maalum na gazeti hili ofisini kwake mwishoni mwa wiki, Kiongozi wa RGC Tabata Chang’ombe Mtume Peter Nyaga, alisema wanajisikia faraja kubwa kama kanisa kutokana na uamuzi wa Waziri Mkuu Pinda, kukubali kufika katika sherehe hiyo ya kihistoria katika kanisa lao.

“Sisi kama kanisa tumefurahishwa sana na uamuzi wa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, kukubali kushiriki katika sherehe yetu hii, tunajivunia kuwa naye katika siku hii ambayo inaakisi harakati zetu za kumtumikia Mungu ambazo zimekuwa na mafanikio makubwa tangu siku niliyoitwa kwa ajili ya kumtumikia Bwana katika nchi hii” alisema Mtume Nyaga.

Alisema pamoja na kupitia changamoto nyingi ikiwemo kufungwa jela kwa sababu ya kumtumikia Mungu, lakini wanashukuru kwa sababu Mungu amekuwa pamoja nao na kuwafanikisha kwa kiasi kikubwa katika kipindi chote cha miaka saba ambacho kimeshuhudia maelfu ya watu wakikombolewa kutoka katika utumwa wa shetani na kurejeshwa katika ufalme wa Mungu.

Tangazo limetengenezwa na Rumafrica +255 715851523

Kwa mujibu wa Mtume Nyaga, sherehe hiyo ya kihistoria itatanguliwa na semina maalum ya uumbaji na maajabu, itakayofanyika Jumapili ya leo ni kuanzia saa 3 asubuhi hadi 6 mchana na kuanzia Jumatatu mpaka Ijumaa semina itafanyika kuanzia saa 9 alasiri hadi saa 12 jioni. Alisema Semina hiyo itahitimishwa kwa sherehe kubwa ya kanisa itakayofanyika siku ya Jumamosi tarehe 7/12/13 kuanzia saa 5 asubuhi hadi saa 12 jioniambapo Mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Kayanza Peter Pinda (MB).

Akiingumzia siku hiyo, Mtume Nyaga alisema, itahusisha mambo kadhaa ikiwemo Kutimiza miaka saba (7) ya Kanisa, kufanya tendo la huruma la kula chakula cha mchana na watoto yatima, walemavu na wajane, kuzindua Vitabu 7 vya Urejesho vilivyoandikwa na Mtume na Mchungaji Peter Njue Nyaga kwa neema ya Mungu ili viwe Ukombozi kwa jamii ya Watanzania na kuwagawia chakula, walemavu, watoto yatima na wajane.

Alivitaja vitabu vitakavyozinduliwa siku hiyo kuwa ni pamoja na Nguvu ya Kibali, nguvu ya uponyaji, Nguvu ya Imani, Nguvu ya Urejesho, Nguvu ya Roho Mtakatifu, Nguvu ya Fedha na Nguvu ya Ujasiriamaliambavyo anaamini kwa neema ya Mungu endapo vitatumika vizuri vitaleta mabadiliko makubwa katika maisha ya wanadamu.

Mtume Nyaga, alisema lengo la uzinduzi huo utakaohudhuriwa pia na Askofu Mkuu wa RGC Duniani Dokta Arthur Kitonga, ni kwa ajili ya kutoa sadaka maalum ya ununuzi wa lori la kuhubiria injili vijijini ili kuwafikia ambao bado hawajafikiwa na Injili ili wengi wapate kuona matendo makuu ya Mungu ya kuokolewa, kuponywa na kufunguliwa kutoka kwenye vifungo mbalimbali vya shetani.


Alisema baada ya kuhubiri injili kikamilifu katika jiji la Dar es Salaam na kufanikiwa kuokoa watu wengi, sasa ni zamu ya mikoani na hasa vijijini kwenye uhitaji mkubwa wa injili, hivyo alitoa wito kwa wote wanaopenda kushiriki Baraka hizo kwa kuchangia kupatikana kwa lori hilo kutuma sadaka zao kupitia Mpesa 0756-863528/ Tigo pesa 0716147361 au wafike siku ya tukio na Mungu wa mbinguni atawabariki.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...