Jina langu la passport ni
Rulea Sanga, niliyezaliwa Makete miaka ya iliyopita, na baada ya hapo
mama yangu amabye ni marehemu kwa sasa, alihamia katika kijiji cha Mtili
"A" ambako mimi na mama yangu tukaweka makazi hapo. Nimesoma katika
shule ya Msingi mtili "A" na kumaliza darasa la saba hapo hapo kijijini.
Namshukuru Mungu baada ya kumaliza nikajiunga na sekondari mji
fulani na baadae kuhamishiwa Njombe Sekondari na hapo ndipo nilimaliza
kidato cha nne...
Mungu hakutaka niishie hapo ndipo nilipojiunga
na kidato cha sita shule ya sekondari Jitegemee jijini Dar es
Salaam....kitabu kilikuwa tough kidogo lakini Mungu alinipigania..
Yehova
akazidi kufungua milango yangu nikasoma kompyuta IIT jijini Dar es
Salla na kubeba International Advance Diploma in Computer Studies..Siku
hiyo ilikuwa furaha kwangu...
Mungu akanitoa utandu wa giza
machoni pangu na kunipeleka katika Chuo Kikuu cha Usimamizi wa Fedha
IFM jijini Dar es Salaam ambapo niliinuka na gamba la mambo ya Hifadhi
ya Jamii (Social Protection)...Mungu wangu nakupenda!!!
Nikaingia mitaani....hapa kuna mambo mengi nilipitia katika maisha...sipendi nikuchoshe...
Lakini
leo hii Mungu akanipa kibali cha ajabu sana. Kwako muujiza huu unaweza
kuonekana wa kawaida ila kwangu ni mkubwa sana, nikilinganisha na
nilikotoka na nilipo ni kwa neema ya Mungu. Nikiwa katika maisha ya
kujaa funza na taa ni kibatali, moshi wa jikoni kwangu ilkuwa kawaida
sana....ni mengi rafiki yangu.
Nakumbuka mwezi mmoja hivi
umepita niliambiwa nitegeneze blogu wa COME AND SEE PROMOTER, na baada
ya kumaliza mimi nikawa ni mtu kuwaelekeza wageni rasmi waliokuja
kuzindua hiyo blogu...Mimi kwangu mimi ni maajabu, kwani wapo wangapi
wametoka kijijini kama mimi na hawajafanya mambo kama haya na wako mjini
hapa. Ninachoamini katika maisha ni kuwa karibu sana na Mungu, naye
atakuinua kutoka chini na kwenda juu. Na usiwe na haraka ya maisha, wewe
kaa miguuni pa Mungu Baba na ukijibidiisha kikazi...Mungu akubariki.
Kutoka Kushoto Jerry
Muro,Rulea Sanga(Blog Designer),Mgeni Rasmi,Afande Eva,Mchungaji,Emmanuel Na Mc
Chavala
" Tamasha Hili Lilikuwa Na Malengo Makuu Matatu,1.
Kutambulisha Na Kuuza Maono Ya Come And See Hapa Tanzania 2. Kuzindua Blog Yake Na
3. Kukusanya Pesa Za Kuandalia Tamasha Maalum La Walemavu Wenye Vipaji
Litakaloitwa "Wapende Walemavu" Na Kwa Kwa Hakika Mambo Hayo
Yalifanikiwa!!"
Mc Chavala kushoto
Hapa unamuona mgeni rasmi pamoja na wageni maalum wakifuatilia yanayoendelea kwa makini kabisa!!!
No comments:
Post a Comment