RUMA AFRICA INVITE YOU TO WATCH EMMANUEL TV -TB JOSHUA LIVE

Sunday, November 25, 2012

CHOZI LA MTOKA RULEA SANGA KATIKA KANISA LA EFATHA MWENGE-DAR KWA MTUME NA NABII JOSEPHATE MWINGIRA


Kuna siku huwa naenda kanisani lakini leo ilikuwa siku “Special” kwangu katika nyumba takatifu ya MUNGU Efatha kwa Nabii na Mtume Josephate Mwingira. Mahubiri na maombezi ya leo yamenigusa sana mpaka chozi langu likadondoka. Baada ya kuona hivyo nikaamua kukushirikisha na wewe mdau wa RUMAFRICA ili upate upako wa Jumapili hiii. Na hivi ndivyo Nabii na Mtume Josephate Mwingira alivyoanza kulisha kondoo wake Mwenge Dar es Salaam katika kanisa lake lenye upako wa ajabu.

Creative Director-Rumafrica, Rulea Sanga

”Leo ni siku ya maajabu kwa maana MUNGU anajibu maombi ya yule aombaye. Utaona utukufu wake siku ya leo kwa kumwamini huyu MUNGU. Mwaka huu utaona maajabu unachotakiwa ni kutokata tama na usisikilize ya watu, bali sikiliza YESU anasema nini juu yako. Yupo MUNGU wetu kwahiyo huhitaji kulia na kutoa machozi. Wewe endelea kumpenda MUNGU, na Mungu anaendelea kukupenda kwasababu ubafuata yale YEYE anakuambia.. MUNGU anaendelea kukupeleka mahali pa juu nay ale yaliyokukundamiza yatapotea. Usiende kama unavyojisikia ila nenda kama MUNGU apendavyo, kwa kuwa mwaninifu katika njia zake.

Ni mahali pamoja tu unweza kufikia amani na furaha, na hapo ni mbele ya YESU. Dunia imejaa maovu, MUNGu wa mbinguni anakutakia mema na mafanikio, hapendi kuona mwanae unalia na kuteseka. Wengine wanateseka na kulia kutokana na taabu za duniani ni kutokana na kumpenda MUNGU nusu na nusu nyingine ni kwaajili ya dunia..Ndugu yangu ukitarajia mazuri kwake utapata mazuri. Mtazame Yesu na usitoe macho yako kwa YESU. Yesu anasema usitarajie kupitia magumu, ila utayashinda katika YEYE.

Unaweza kuchangia kupita katika matatizo kwa kutokuwa na adabu ya KIROHO. Ipo siku dunia itaondolewa na waliokufa watakuwa mahali Fulani na walio hai watakuwa mahali Fulani, dunia itakuwa imekunjwa nama karatasi na kutupwa motoni. Wakati dunia imekunjwa, walioko makaburini wataondolewa ili wahukumiwe. Waovu watakusanywa pamoja nakuhukumiwa.

Sio wote waliokoka kanisani wataenda mbinguni kwani kuna wengine hawaamini maneno ya mitume wake walioko duniani na waliotumwa na MUNGu kwa kazi yake. Hata kama wanamwamini MUNGU lakini itakuwa ngumu sana kwao kumuona MUNGU kama hawataamini ya mitume. Kipindi cha YESU, kuna watu walitumwa na kuwekewa wakfu kwaajili ya kazi ya MUNGU. Kuna wahibiri wachache sana wametumwa kubeba watu WAKE. Eliya alilia sana akiomba MUNGU kuwa anapowaondoa wengine na yeye awemo katika kundi. Unatakiwa na wewe kulia pale MUNGU atakapokuwa anawachukua walio wake na wewe uwepo.

Ifike mahali YESU anapoondolewa na wewe pia uondolewe. Kwa macho ya kawaida YESU huwezi kumuona kwa macho ya KIMUNGU unamuona. Paulo alisema nifuateni mimi kama ninavyomwamini KRISTO, na ninaomba mniamini na mimi kwa maana sitowapoteza. Ninawaomba wana Efatha muniamini na mimi Mtume na Nabii wenu wa kizazi hiki, Josephate Mwingira sitawapoteza kamwe.


Kuamini kitu usichokiona ni kazi sana kwani hukioni, ial mimi naonekana madhabahuni hapa kama Nabii wenu. Unaweza kuona Josephate Mwingira anapiga porojo madhabahuni ila ana kitu unachokihitaji katika maisha yako, sasa kama humwamini hutakipokea kwa maana utamuona kama tapeli anakutapeli.


SOMO LA JUMAPILI

ROHO BWANA YU JUU YANGU
Huu ni mwendelezo wa masomo yaliyopita wiki zilizopita na leo tutasoma Luka 4:18, “Roho wa Bwana yu juu yangu kwa maana amenitia mafuta kuwahubiria maskini habari njema, amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao na vipofu kupata kuona tena na kwacha huru waliosetwa.”

Pepo kuondoka sio kuwa umeokolewa. Neno ndilo linakufanya kuondoa ulipokandamizwa. Neno likikolea kwako baada ya kufundishwa utapata kuona, na ukishaona unapata ufunuo ambao unakusaidia kuona ujanja wa shetani na mafundisho ya shetani

Shetani anapoona umefanya mambo yake, unatakiwa kuzidi kuwa na YEYE ili shetani asikufunge.

Kitu tunachopewa ni kufika mahali huru na kuona kile shetani anafanya juu yetu. Tunapoona ujanja wa shetani tunaweza kuweka watu huru. Unawafungua watu, wanaweza kuona tena.

Kuna mambo matatu yanayohusiana na kuona ila tutazungumizia haya mawili:
  1. Mungu anafanya nini, na alifanya nini?
  2. Mungu alimaliza kazi yake
  3. Mungu ameona nini, na aliona nini?

MUNGU ANAFANYA NINI NA ALIFANYA NINI?
Tusome Mwanzo 1:1 na 2:1-2 na Methali 8:22-26 na Yohana 1:1-3] Mungu aliumba kila kitu hapa duniani. Unapoona kila kilichopo hapa duniani, unaona ni nani alifanya. Aliyefanya vyote hivyo ni Mungu mwenyewe.

MUNGU ALIMALIZA KAZI YAKE.
Unatakiwa kujua kuwa kila kitu unachofanya, utakimaliza kwa ushindi kwani YESU alimaliza kazi yake msalabani kwa ushindi. Unachotakiwa ni kuamini kuwa utamaliza yale yote uliyoyapanga. Ondoa mashaka ila angalia MUNGU anafanya nini juu yako. Unapoanza jambo sahau kabisa ila fikiria kushinda na amini kwa hilo. Usiangalie watu wanasema nini, usijilinganishe na watu wengine ila tuamainia kwa MUNGU. Kama wewe ni wa kanisa la EFATHA, hakuna atakaye kumaliza na wakitaka kukuloga itashindikana, ule uwepo wako kwa adui zako utakuwa ndio uchawi wako kwa adui zako. MUNGU anaenda kukutumia wewe kuwa fimbo na rungu la kutwanga maovu.

Mungu anasema amekuweka ishara na watakaokuongelea jina lako ili lisifike mahali unapotaka kufika, watashangaa ukichomoza. Kama una duka karibu na mchawi wako utashangaa watu wakija kukuona maana huyo mchawi ataondolewa nah ii itasababisha watu kuja kushangaa jinsi ulivyomtoa huyo mchawi.

Ondoa hofu ya kuwa utashindwa bali nenda ukaanze kwa kishindo. Kushindwa kwako kuanzia leo nakutamkia itakuwa kama kaskazini na Kusini kwani  MUNGU anayaweza katika yeye atutiaye nguvu. Unatakiwa kumtukuza MUNGU kwani anakuwezesha. Kama wewe uliomba MUNGU akusaidie jambo, atakuzidishia. Tangia umezaliwa unateseka, lakini sasa yote yamekwisha

MUNGU AKUBARIKI

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...