RUMA AFRICA INVITE YOU TO WATCH EMMANUEL TV -TB JOSHUA LIVE

Friday, December 14, 2012

MTANGAZAJI WA CHANNEL TEN, BONIFACE MAGUPA SIKU YA JUMAPILI ALIVISHA PETE MCHUMBA WAKE JESSICA HONORE KATIKA KANISA LA WORDALIVE SINZA MORI DAR ES SALAAM


Jana ilikuwa ni siku ya kihistoria kwa Boniface na Jessica baada ya kufanya uamuzi wa busara wa kuvisha pete mbele za Mchungaji wao Deo Lubala. Ilikuwa furaha sana katika kanisa la WordAlive. Kama unavyojua Jessica Honore ni mwimbaji wa nyimbo za Injili hapa Tanzania, na alikuwa katika wazo zito akijiuliza ni lini mzee mzima atamvisha pete.
Watu walikuwa ni wengi sana kuwa-support maharusi hawa watarajiwa. Kulikuwa na Mkurugenzi wa Global Publisher-Shigongo, Mkurugenzi wa Rumafrica-Rulea Sanga, MD wa Glorious Celebration-Emmanuel Mabisa, Mwimbaji nguli-Robert David, Watangazaji wa Wapo Radio-Mbise na Chiwalo, Mchekeshaji Chavala, Mtangazaji wa Praise Power-Kisaka, Mchungaji Deo Lubala wa WordAlive na wengine wengi
 Boniface Magupa akiwa na mpenzi wake Jessica Honore
 Jessica Honore akiwa anawacheki mabesti huku akiwa ameshikilia pete yake ya uchumba
Boniface Magupa hamini kilichotokea katika maisha yake..Kakaaaa huyo wako....
 Na hawa pia walikuwa wakivishana pete ya uchumba
 Mwimbaji wa nyimbo za injili Tanzania, David Robert ambaye ni classmate wa Mkurugenzi wa Rumafrica, Rulea Sanga- enzi hizo ndani ya Jitegemee High school, hapa anaonekana akitoka kumpiga picha Boniface na mchumba wake.
 Mchungaji Deo Lubala akiwaombea Bwana na Bibi harusi watarajiwa
Boniface Magupa akiwa makini kumsikiliza Mchungaji wake Deo Lubala akiwapa husia

Kutoka kulia wa nne ni mkurugenzi wa Global Publisher, Erick Shigongo akiwa katika picha ya pamoja
 Boni
Waliosimama ni Bwana harusi na Bibi harusi watarajiwa ambao siku ya Jumapili walivishana pete ya uchumba
 Mtangazaji wa Channel Ten na Bwana harusi mtarajiwa Boniface Magupa akiwasiliana na mtangazaji radio ya Wapo, Chiwalo (kulia)
 Jessica Honore akihagiana na rafiki yake
 Picha ya pamoja
 Duhu Mkurugenzi wa Rumafrica alivyo rafu...hajui hata mitoko..kweli yuko kikazi. Unayemuona katika picha hiii ni rafu ni Rulea Sanga.
 Boniface Magupa akiwa na jamaa na marafiki
 Kutoka kulia ni mwimbaji mkongwe wa nyimbo za injili Tanzania, David Robert
 Mchekeshaji Chavala akiwa na Bwana harusi na Bibi harusi watarajiwa

Mwimbaji wa nyimbo za injili Makondeko (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wahusika wenyewe
 Ni kujiachia tu...kwani wamefanya yao..na sisi tufanye yetu.
 Mkurugenzi wa Rumafrica Rulea Sanga akiwa na Mkurugenzi wa Global Publisher Erick Shigong
 Cahala na Erick Shigongo

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...