Mungu yuko
upande wako.
Na hilo linapita mama yangu,
Hakuna
jambo linalodumu hapa chini ya jua.
Hata kama
jaribu lako liwe kubwa, ufananishe na Mlima Kilimamjaro.
Ila ninajua
ipo siku moja ninakuambia, mbele ya macho yako hilo jaribu litatoweka.
Namshukuru sana Mungu kwa yale anafanya juu ya maisha yangu. Umekuwa mwema sana BABA..nilikupenda, ninakupenda na milele yote. Asante hata kwa mahali hapa uliponipa pa kuishi.
Jipe moyo
katika jaribu unalopitia, maana kila jaribu lina mlango wa kutokea.
Mbona wewe
moyoni mwako unaumia, machozi machoni pako yanatairirika, kwa jaribu
unalopitia, unadhani Mungu kakuacha. Mungu hajakuacha hilo jaribu ni la muda tu.
Mungu ndiye
aliyesema, hata upitapo katika maji mengi hayatakugharikisha.
Mungu
hawezi kukuacha na hilo
jaribu likupoteze.
Nina kwa neema ya mkombozi, ni neema sikustahili. Nimefanyika kuwa mwana na nimehesabiwa haki.
Uwe mtu wa imani mpendwa wangu. Karibu nyumbani kwa Yesu utaona mkono wake.
Jaribu
unalopitia lisikutoe kwenye imani, kwani Mungu hajashindwa.
Yawezekana
ni magonjwa yanakusumbua. Umezunguka hospitali zote na hujapona.
Yawezekana
ni ndoa yako inakusumbua, unatamani hata kuachana inashindikana.
Yawezekana
ni maisha mipango haiendi, kila unalolipanga kwako linashindikana.
Yawezekana
ni watoto wanakusumbua, hawataki shule na hawakusikii..wameshindikana.
Yawezekana una elimu nzuri lakini kazi huna, umezunguka
kutafuta kazi sasa umechoka ma viatu vimeisha
Umekata tama
huna la kufanya. Usipoteze tumaini lako, Mungu anaweza.
Mungu huyu
anayembariki yule, ndiye atakayekubariki na wewe. Mungu yule anayemponya yule
ndiye atakayekuponya. Mungu yle anamsaidia mtu kuwa na nyumba yake ya kuishi
ndiye yule atakae kupa nyumba ya kushi. Mungu yule anayempa yule mke au mume,
ndye atakayekupa mume au mke. Mungu yule anafanya connection na watu
waliobarikiwa na kuwa na mali
nyingi, ndiye atakaye kuunganisha na watu wakubwa. Mungu akuti nguvu mpendwa
wangu unayepitia katika magumu na umekata tamaa.
FANYA YALE
MUNGU ANATAKA UFANYE, UTAONA NEEMA YA MUNGU
No comments:
Post a Comment